HII NDO ATHARI YA KUWEKA PICHA ZA UCHI MTANDAONI



Mwezi wa kujistiri kwa wale wenzangu na mie ndiyo huo umeondoka, hapana shaka kuna wengine wanasoma hapa, huku wakiwa ndani ya yale mambo yetu. Siyo ishu, kila mtu ana uhuru wa kufanya kile akipendacho. Nchi yetu inaruhusu kuvaa chochote, ilimradi tu usiende utupu.

Nakumbuka miaka kama mitatu nyuma iliwahi kutokea hoja kuhusu mavazi, wengi walisema Serikali ilikuwa na mpango wa kupiga marufuku vimini na nguo za kubana.



 Basi bwana siye tunaopenda mambo hayo roho zilikuwa juu, huku wengine tukitishia hata kuhama nchi ikiwa tutafikia huko kwa kukatazana mavazi.

Lakini kwa bahati nzuri rais wetu, Jakaya Kikwete alilitolea tamko suala hilo  na kusema kuwa kila mtu ana uhuru wa kuvaa kile anachojisikia, ili mradi tu asiende utupu. Hapo alimaliza kila kitu.

Tuachane na mambo ya mavazi, suala la msingi leo ni ‘mapicha’ na tattoo tunazochora mwilini na kuzitupia mtandaoni kila kukicha. Turudi kulekule kwenye uhuru wa kufanya kile unachojisikia, lakini usiku ukienda kulala jiulize mwisho wake nini?
Mimi na wewe hatujui kesho tutakuwa kina nani katika dunia hii, labda uniambie wewe huna ndoto za kufanya jambo litakalokufanya ukumbukwe, hata ukitoweka kwenye uso wa dunia.

Kila mtu, hasa wasichana waona fahari kuweka picha za nusu uchi  katika mitandao ya facebook, twitter na sasa instagram . Ujana, maji ya moto, kwa sasa hizo ‘likes’ na ‘comment’ unazopata zinakuvimbisha kichwa, lakini naamini baadhi yetu, miaka kumi ijayo tutatamani kurudi nyuma ili tuondoe historia mbaya tulioiweka mtandaoni.

Picha hizi zitatumika kukugandamiza kwa chochote unachokusudia kukufanya wakati huo. Ni nani atamchagua kiongozi mwenye picha kama zako unazotupia sasa.Kampuni gani yenye heshima itakayomwajiri mtu mwenye sifa mbaya kwa jamii.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates