SIRI YA MCHEZO LYRICS
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo…
stimu zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans
wanascream nikirap../ sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream
hiphop/
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teamMabiiitoz /
Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/ na umaarufu au kutamba.. kushika namba
ni bahati..sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu/ kisa track
ikivuma sana kwenye chati haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../ baba asante kwa UTAFITI
na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya
MARIJANI../ najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu
zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../ inasikitisha
unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
‘’Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye
siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../
huo ni utumwa pia/Unafanya vijana wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment