Latest Updates

MICHEZO - KUELEKEA DAR DERBY OCTOBER 1 KOCHA YANGA AMEONGEA HAYA

11:36 PM

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi ameanza kupandisha homa ya pambano la watani wao Simba baada ya jana kujinasibu kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo utakaochezwa Oktoba Mosi, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mwambusi alisema timu yake haipewi nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na kiwango wanachokionesha Simba kwa sasa kwenye mechi za Ligi Kuu lakini amewahakikishia mashabiki wao kuwa lazima washinde.
“Kama kuna watu wanafikiri tutapoteza mechi yetu dhidi ya Simba, Oktoba Mosi wanajidanganya, mashabiki wetu wasiwe na presha tuna wachezaji wazuri kuliko hao wa Simba na muda ukifika kila mtu ataona kitakachotokea Taifa,” alisema Mwambusi.

Pia Mwambusi alisema beki Andrew Vicent ‘Dante’ yupo vizuri hivyo ukuta wao hautapenyeka kirahisi japo itakuwa mechi yake ya kwanza dhidi ya Simba ila kwa kuwa wamejiandaa vya kutosha wamejipanga kushinda.

Mwambusi alisema Dante ana uwezo wa kumdhibiti mshambuliaji mpya wa Simba raia wa Burundi Laudit Mavugo na asilete madhara kwenye lango lao kutokana na umahiri wa nyota wake.

Simba inaongoza katika msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia pointi 13 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 10 huku wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja baada ya kushuka dimbani mara nne.

PICHA - NOMINATION WA MTV MAMA WAKO HAPA

10:44 PM

Ni Sept 21, 2016 ambapo majina ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016 yalitajwa huku Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na kundi la Navy Kenzo pamoja  na Alikiba ndio wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo kubwa za Africa za MTV Africa Music Awards 2016.

.

Diamond anawania kipengele kimoja cha Best Male ambacho anachuana na Black Coffee (South Africa), Wizkid (Nigeria), AKA (South Africa),  Patoranking (Nigeria).

.

Navy Kenzo wanawania kipengele cha Best Group ambapo wanachuana na Toofan (Togo) , Micasa (South Africa) , R2Bees (Ghana).

.

Alikiba ametajwa kuwania kipengele cha Best Collaboration kupitia wimbo aliyoshirikishwa na Sauti Sol uitwao Unconditionally Bae.

Kenya imewakilishwa na kundi la Sauti Sol wanaowania kipengele cha Best Group of the Year na Best Collaboration huku Uganda imewakilishwa na Eddy Kenzo  anayewania kipengele cha Best Live Act.

Tuzo hizo zitatolewa Jumamosi ya tarehe 22 October, 2016 huko Johannesburg, Afrika Kusini na tukio hilo kuoneshwa moja kwa moja kupitia channel ya MTV Base.

Hii ni orodha kamili:

Best Live Act

Stonebwoy (Ghana)

Cassper Nyovest (South Africa)

Mafikizolo (South Africa)

Mr Flavour (Nigeria)

Eddy Kenzo (Uganda)

Best POP/ ALtenative

Tresor – Never let Me Go

Shekinah & Kyle Deutsch- Back to the Beach

Timo ODV- Find My Way

LCVL ft Sketchy Bongo- Cold Shoulder

Desmond  & The Tutus – Pretoria Girls

Personality of the Year

Caster Semenya

Linda Ikeji

Pearl Thus

Wizkid

Pierre Emerick

Best Group

Toofan (Togo)

Micasa (South Africa)

Navy Kenzo (Tanzania)

R2Bees (Ghana)

Sauti Sol (Kenya)

Best Male

Black Coffee  (South Africa)

Diamond Platnumz (Tanzania)

AKA (South Africa)

Patoranking (Nigeria)

Wizkid (Nigeria)

Best Lusophone

NGA

Nelson Freitas

C4 Pedro

Lizha James

Preto Show

Best International Act

Beyonce

Drake

Adele

Future

Rihanna

Best Collaration 

AKA ft Yanga, Burna Boy, Khuli Chana -Baddest

Dj Maphorisa, ft Wizkid, Dj Buckz- Soweto Baby

Nasty C ft Davido, Cassper Nyovest – Juice Back Remix

Sauti Sol ft Alikiba – – Unconditionally Bae

Patoranking ft Sarkodie  -No Kissing

Best Hip Hop

Emtee (South Africa)

Ricky Rick (South Africa)

YCEE (Nigeria)

Olamide (Nigeria)

Kiff No Beat (Ivory Coast)

NIMEKUSOGEZEA HAPA MAGAZETI YA UDAKU NA MICHEZO

10:35 PM

September 22 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzaniakuanzia kwenye, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea


PICHA - WANAUME WA JAPANI WAMESOMA KOZI HII ILI KUVUTIA WANAWAKE

10:29 PM

Najua kuna watu wangu ambao sasa wapo kwenye mchakato wa kuoa au ndio wanatafuta mtu ambaye wataishi nao, lakini inawezekana kumekuwa na changamoto, Sasa leo September 20 2016 nakusogezea hii inayotokea nchini Japan ambapo wanaume ambao bado hawajaoa wanahudhuria kozi ya kulea watoto ili kumvutia mwanamke zaidi.

Bachelor hao wa kijapan wamehudhuria kozi ya kulea watoto ili kuongeza nafasi ya wao kupata wapenzi, Mwalimu wa kozi hiyo Takeshi Akiyama amesema lengo la kozi hiyo ambayo imeandaliwa na Ikumen University ni ili kusaidia mtu ambaye hajaoa kupata mke.

Masaya Kurita (31) bachelor anayeishi Tokyo Japan ameanza kozi baada ya kutafuta mke kwa miezi sita iliyopita, Aidha anaamini kuwa kufanya mazoezi ya kulea mtoto kwa kutumia plastiki kunaboresha nafasi yake ya  yeye kukukbalika kwa mpenzi .

NEWS - MTEMVU ASHINDWA KESI YA UBUNGE TEMEKE

10:26 PM

Aliyekuwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abbas Mtemvu, ameshindwa kesi ya uchaguzi dhidi ya Abdallah Mtolea(CUF) aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.

Mtemvu aliyekuwa akitetea kiti hicho katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alifungua kesi  katika  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akipinga matokeo yaliyompa ushindi  Mtolea.
Pamoja na mambo mengine akidai kuwa kura  za baadhi ya vituo vya kupigia kura hazikujumlishwa katika matokeo ya jumla.

Hata hivyo Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa   na Jaji Issa Maige aliyekuwa akisiliza kesi hiyo imetupilia mbali madai ya Mtemvu na badala yake imemthibitisha Mtolea kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Katika hukumu hiyo Jaji Maige amesema kuwa Mtemvu ameshindwa kuthibitisha madai yake jinsi yalivyoathiri ushindi wa mbunge huyo, huku akisema kwamba kasoro alizokuwa akizilalamikia Mtemvu hakuathiri ushindi wa mbunge huyo.

News wasiokua na uraia wajadiliwe

10:23 PM


Tanzania  imeitaka jumuiya ya  kimataifa   kujadili  tatizo  la  uwepo wa watu  ambao si raia wa nchi  yoyote ile.

Pendekezo hilo limetolewa siku ya  Jumanne na Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Dkt. Augustine Mahiga ( Mb)    katika  mkutano     wa  Kilele wa  viongozi  kuhusu wakimbizi.

Mkutano huo  uliandaliwa na  Rais wa Marekani Barack Obama  kwa  ubia na nchi za  Ethiopia, Jordan, Mexico, Sweden, Canada  na Ujerumani  ambapo nchi  60  zilialikwa,45 kati ya zilizoalikwa ikiwamo   Tanzania    zilitoa ahadi ya  namna moja ama  nyingine. 

Nchi  hizo ni zile ambazo kwa namna moja ama nyingine   zimekuwa zikiwapokea na kuwahifadhi wakimbizi,  zimekuwa nchi za mpito kwa wakimbizi, au zimekuwa  zikitoa misaada   ikiwamo ya  hali na mali pamoja na kuwapatia uraia, ajira na  misaada ya kibinadamu.

Lengo kuu la mkutano  huo wa  viongozi kuhusu wakimbizi lilikuwa ni kwa nchi kutoa ahadi mpya ambazo  kwayo  zitasaidia katika  kuwapatia fursa za ziada  wakimbizi ili  pamoja na mambo mengine kuwapunguzia changamoto zinazowakabili na kuwafanya wajisikie na kujiona  kuwa  nao ni  binadamua kama  binadamu  wengine.

Akizungumza kwa  niaba ya Serikali,   Waziri Mahiga, amesema, Tanzania  kutokana na jiografia ya nchi hiyo  ilivyo imejikuta  mara kwa mara ikiwa ni kimbilio  la wakimbizi kutoka  nchi jirani.

Akawaeleza  washiriki wa mkutano huo, kwamba, suala la  Tanzania  kuwahifadhi  wakimbizi ni la kihistoria na  halikuanza  jana au juzi.

“ Tanzania kutokana na jiografia yake imejikuta  ikiwa ni kimbilio wa watu wanaotafuta salama ya maisha yao. Tumekuwa  tukiwapokea na kuwahifadhi wakimbizi  tangu miaka  ya 60.  Na  tunatekeleza   jukumu hilo kwa kuzingatia sheria  za kimataifa na mikataba ya kimataifa, na sheria zetu za ndani” akasema Mahiga.

 Na kuongeza kwamba, Tanzania itaendelea na jukumu hilo pale itakapopashwa  kufanya   hivyo kwa  kufuata na kuzingatia sheria  za nchi na  sheria za kimataifa.

CHIWILE INC IS BACK

7:42 AM

Chiwileinc is Back! Kaa tayari

NEWS - Serikali yasisitiza dhamira yake kuhusu ndoa za utotoni

11:52 AM

August 19 2016 Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto amefanya uzinduzi wa mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya II jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mwalimu amesisitiza dhamira ya Serikali ni kuendeleza jitihada za kufanya marekebisho ya sheria ya ndoa ya mwaka 1997, hususan katika kifungu 13 (1) cha sheria ya ndoa kinachoeleza kuwa umri wa mtoto wa kike kuolewa ni kuanzia miaka 15.

Aidha Waziri Mwalimu ametoa ufafanuzi zaidi kuhusu Serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu kuhusu sheria hiyo kuwa ni ili kupata maamuzi ya juu zaidi ambayo hayataweza kupingwa na mahakama nyingine ya chini.

NEWS - VIPENGELE TUNZO ZA EATV AWARDS VIKO HAPA

11:45 AM

Vipengele vya tuzo mpya zilizoanzishwa na kituo cha runinga cha East Africa Televisheni, EATV Awards, vimetangazwa Ijumaa hii.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Mkuu wa masoko wa kituo EATV,Roy Mbowe alisema tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.
Vipengele hivyo ni:

1. Mwanamuziki bora wa kiume
2. Mwanamuziki bora wa kike
3. Mwanamuziki bora chipukizi
4. Kundi bora la muziki
5. Video bora ya muziki
6. Wimbo bora wa mwaka
7. Muigizaji bora wa kiume
8. Muigizaji bora wa kike
9. Filamu bora ya mwaka
10. Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.

Mbowe amesema kazi za sanaa zitakazoruhusiwa kuingia kwenye vipengele ni zile zilizotoka kuanzia Julai 1 2015 – 30 Juni 2016. Tofauti na tuzo zingine, wasanii wanaotaka kushiriki watalazimika kujaza fomu za kutaka kutajwa kwenye tuzo na kuwasilisha kazi husika ambapo mchakato wa uchambuzi wa kazi hizo utachukua kipindi cha mwezi mmoja kabla ya majina yaliyoingia kwenye tuzo hizo kutajwa na kuanza kupigiwa kura.

Hata hivyo amedai kuwa pamoja na wananchi kupiga kura, kutakuwepo na jopo la majaji litakaloshiriki kupata washindi. Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

RAZA LEE KUMALIZANA NA TAIFA YA JANGOMBE JUMAMOSI SAA 3 ASUBUHI, APANIA KUINUNUA KWA SHS MILIONI 35

7:12 AM

Mohd Ibrahim “Raza Lee” siku ya Jumamosi ya tarehe 30 July anatarajia kuinunua timu ya Taifa ya Jangombe kwa shs Milioni 35.

Leo Usiku atafunguka LIVE kupitia kituo cha Radio cha Coconut FM 88.9 kwenye kipindi chao cha Coco Sports kuanzia saa 2:00 za usiku.

TETESI ZA SOKA ZANZIBAR LEO JULY 28, 2016

7:07 AM

Adeyum Saleh afagiliwa usajili wake wa kwenda Stand United, Wakala wa Mchezaji mpya wa Stand United Saleh Machupa ambae pia ni baba mzazi wa mchezaji huyo amesema mtoto wake amekwenda timu sahihi na yeye ndio aliemshauri kwenda timu hiyo baada ya kuondoka Coast Union ya Tanga ilioteremka daraja.

Mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Suleiman Hamad ambae kwasasa anacheza timu ya Kijichi anatarajiwa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na moja ya timu ya Ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwemo Mtibwa Sugar , wakati huo huo pia huwenda akarejea timu yake ya Zamani ya Black Sailors.

Timu ya Small Renger inayoshiriki ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini ipo mbioni kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Hafidh Ali “Mess wa Makadara” kwa gharama yoyote kutokea klabu yake ya sasa ya Muembe ladu.

Yahya Haji “karoa” mshambuliaji wa Villa United “Mpira Pesa” anawindwa na timu ya KVZ na JKU, mchezaji huyo amezisaidia kuzipa ubingwa wa Rolling Stone timu ya Mjini Zanzibar na Villa United Daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Mashabiki wa Soka Visiwani Zanzibar wameipa tano timu ya Kombain ya Mjini Zanzibar baada ya kuonesha soka safi katika mchezo wa kirafiki uliosukumwa jana usiku kwenye uwanja wa Amaan ambapo timu hiyo imepigwa 1-0 na Azam FC.

Mohd Ibrahim “Raza Lee” siku ya Jumamosi ya tarehe 30 July anatarajia kuinunua timu ya Taifa ya Jangombe kwa shs Milioni 35. Leo Usiku atafunguka LIVE kupitia kituo cha Radio cha Coconut FM 88.9 kwenye kipindi chao cha Coco Sports kuanzia saa 2:00 za usiku.

Utafiti- Unajua watu walefu zaidi wanapatikana wapi?

7:28 AM

Utafiti mpya umeonesha kwamba wanaume wa Uholanzi ndio warefu zaidi duniani, na upande wa wanawake, wanawake wa Latvia ndio warefu zaidi.

Kimo cha wastani kwa wanaume Uholanzi ni futi 6 kwa sasa (sentimeta 183), na kimo cha wastani kwa wanawake wa Latvia ni futi 5 inchi 7 (sentimeta 170).

Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa kwenye jarida la eLife, umefuatilia kimo cha watu na mabadiliko yaliyotokea katika mataifa 187 tangu 1914.

Utafiti huo umebaini kwamba wanaume wa Iran na wanawake wa Korea Kusini ndio walioongeza kimo zaidi, wakiongeza kimo cha wastani kwa zaidi ya inchi 6 (sentimeta 16) na inchi 8 (sentimeta 20) mtawalia.

Wanawake wafupi zaidi duniani wanapatikana nchini Guatemala huku wanaume wafupi wakitokea Timor Mashariki.

Mwanamke wa umri wa miaka 18 kwa wastani nchini Guatemala alikuwa na kimo cha futi 4 inchi 7 (sentimeta 140) mwaka 1914 utafiti wa kwanza ulipofanywa na sasa kiwango hicho hakijafika kabisa futi 4 inchi 11 (sentimeta 150).

Kimo cha wastani kwa wanaume Timor Mashariki ni futi 5 inchi 3 (sentimeta 160).

Watafiti hao wanasema kuwa chembe chembe za jeni hubadilikabadilika, lakini cha muhimu zaidi ni kuwepo kwa lishe bora, usafi na matibabu ya hali ya juu.

Mataifa yenye wanaume warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):

Uholanzi (12)
Ubelgiji (33)
Estonia (4)
Latvia (13)
Denmark (9)
Bosnia na Herzegovina (19)
Croatia (22)
Serbia (30)
Iceland (6)
Jamhuri ya Czech (24)

Mataifa yenye wanawake warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):

Latvia (28)
Uholanzi (38)
Estonia (16)
Jamhuri ya Czech (69)
Serbia (93)
Slovakia (26)
Denmark (11)
Lithuania (41)
Belarus (42)
Ukraine (43)

News- bila wivu hakuna mapenzi jux

10:26 AM

Msanii Jux ambaye sasa ni mpenzi wa Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya 'Wivu' ambao unafanya vizuri kwa sasa hajaimba kwa ajili ya mpenzi wake Vanessa Mdee.

bali ameimba wimbo huo kutokana na hisia kwani jambo hilo linawakuta wengi ambao wanapendana kweli katika mahusiano yao ya kila siku.

Jux akizungumza kwenye kipindi cha ENEWZ ya EATV alidai kwenye mapenzi kama hakuna wivu kati ya wawili wapendanao hapo kunakuwa hakuna mapenzi ya kweli kati yao kwani wivu ndiyo ishara ya upendo wa kweli.

"Wimbo wa Wivu ni matukio ya kimapenzi ambayo yanatokea kwa watu wengi ila siyo kama nimejiimbia mimi, unajua kabla sijarekodi wimbo ule tukiwa studio niliwauliza wakina Bob Manecky na wengine jamanii mnadhani 'idea' hii inaweza kuwa sawa ndipo hapo wakaniambia ni wazo zuri kwani kwenye mapenzi bila uwepo wa wivu kuna kuwa hakuna mapenzi ya kweli, ndiyo hapo nikajua kumbe suala hili linawagusa watu wengi" alisema Jux.

Mbali na hilo Jux amesema kuwa hivi sasa muzuki unakuwa kama haupo kutokana na ukweli kwamba watu wanatanguliza life style mbele kuliko hata kazi zao na ndiyo maana wasanii wengi wakitaka kutoa kazi zao wanafanya mambo mbalimbali kutafuta kiki ili waweze kutambulisha kazi zao hizo.

"Sipendi sana kuulizwa maswali juu ya Vanessa napenda niulizwe maswali juu ya kazi zangu mimi kama msanii, ili nitangaze kazi zangu mimi ndiyo maana kuna vitu saizi sisi tunavikwepa kwa makusudi, tunataka kurudisha muziki hivyo mambo ya kiki, life style tunataka yakae pembeni" alisema Jux

NEWS- watakao sambaza Ky kukiona

4:17 AM

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo yatabainika  yanaendelea   kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, yatafutiwa usajili.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘facebook’.

Alisisitiza kuwa serikali italisimamia suala hilo kwa ukamilifu.

“Sijapiga marufuku matumizi ya vilainishi, ukweli nimepiga marufuku mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kununua na kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao na sababu nimeshazieleza,” aliandika na kuongeza:

“Na nafurahi kuwajulisha kuwa tayari baadhi ya mashirika hayo yameanza kutekeleza agizo hili kwa   kuondoa vilainishi kwenye miradi yao. Nayapongeza sana. Niendelee kuyataka mashirika mengine kutii agizo hili ambalo tutalisimamia kwa ukamilifu.

“Serikali haitasita kuchukua hatua ikiwamo kuyafutia usajili mashirika yanayoendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja”.

Aliyataka mashirika hayo kushirikiana na serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kujikita kwenye afya nyingine  inayozingatia sheria za nchi  na mila na desturi za Watanzania.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Waziri Ummy alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini matumizi ya vilainishi hivyo yanachochea kuongezeka  vitendo vya ushoga ambavyo ni kinyume na sheria za nchi.

“Lengo pia ni kudhibiti maambukizi ya VVU kwa sababu katika   wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, asilimia 23 tayari wana maambukizi hayo.

“Tumebaini baadhi ya wadau wanaotekelezeka shughuli za makundi maalum wamekuwa wakikiuka taratibu za  utendaji na kusambaza vilainishi hivyo.

Awali agizo hilo lilizua mjadala mkubwa katika mitandao ya  jamii, wengi wakikosoa uamuzi huo wa Serikali kupiga marufuku vilainishi hivyo.

Walisema  kwamba vinatumika katika mambo mengine mtambuka hususan hospitalini huku wengine wakisema viendo vya ushoga havichangiwi na kuwapo   vilanishi bali ni mmomonyoko wa maadili uliotamalaki nchini

News- ngumbe & Salu T kuja na ngoma ya pamoja

2:26 PM

Baada ya kila mmoja kufanya poa kwenye ngoma zake artist toka lebo ya mandev records  wameamua kuja na muunganiko usio rasmin baada ya kuamua kufanya ngoma ya pamoja.
Wakiongea na chiwileinc Ngumbe amesema lengo ni kuchanganya mziki wa hip hop wenye ladha tofauti

"Unajua Salu t anafanya hardcore Mimi nafanya comecial  tumeona iv vitu tukiviweka pamoja vitaleta kitu tufauti kwa mashabiki wetu"

VIDEO - DIAMOND FT P SQUARE - KIDOGO

7:07 AM

NEW SONG - WISE BOY - KICHEF CHEF

6:57 AM

COVER -JOINT MPYA YA COOLKAKA

6:11 AM

VIDEO - MAJIBU YA MADEE BAADA YA KUAMBIWA ANATOKA NA SHILOLE

8:00 AM

VIDEO - BEEF MPYA TOWN VANESSA MDEE NA SHILOLE ANGALIA VIDEO WAKIPEANA MAKAVU LIVE

7:44 AM
Kwa inavyo onekana kuna beef ya chini chini kati ya shilole na Vannesa Mdee angalia  hizi video  hapa chini
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates